Mke
wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Wazee wa
Viongozi wa Wilaya ya Mkoani Pemba wakati alipowasili katika majengo ya
Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua Mkanyageni kuzungumza na
wanafunzi wa skuli hiyo wa kuwapatia vifaa kwa ajili ya matumizi yao. ya
kila siku skulini hapo.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema
Shein akiwasili katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma
Pindua Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba.
Wananchi wa Wilaya ya Mkoani Kisiwani
Pemba wakimpokea Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,
alipowasili katika Ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua
Mkoani Pemba.
Wanafunzi
wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua wakiimbi wimbo wa Sisi
Sote Tumekomboka wakati wa hafla ya kukabidhiwa Vifaa mbalimbali na Mke
wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, alipofika Skulini hapo.
Mwanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua Ali Shariff akisoma Quran kabla ya kuaza kwa hafla hiyo.
Mwalimu Mkuu wac Skuli ya Sekondari ya
Mohammed Juma Pindua Ali Simai Makame akitowa maelezo ya Skuli hiyo
wakati wa hafla hiyo ya Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,
kukabidhi misaada mbalimbali kwa Wanafunzi wa Skuli hiyo.
Mkurugenzi
Idara wa Idara Sekondari Bi. Idrisa akizungumza wakati wa hafla hiyo ya
kukabidhi misaada kwa wanafunzi wa Skuli hiyo mpya ya Sekondari
Wilayani Mkoani Pemba.
Mke
wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman akitowa nasaha
zake kwa Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua Wilaya
ya Mkoani Pemba wakati wa hafla hiyo.
Mjumbe
wa Umoja wa Wake wa Wawakilishi na Wabunge Bi Asha Shamsi akisalimia na
kutowa nasaha zake kwa Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma
Pindua Wilaya ya Mkoani Pemba.
Mkuu
wa Wilaya ya Mkoani Pemba Mhe Hemed Suleiman akijibu maswali
yaliowakilishwa wakati wa hafla hiyo na Uongozi wa Skuli ya Sekondari
kwa kupata uhaba wa Maji. na kuwalazimu wanafunzi kufuata maji katika
maeneo ya nje ya skuli yao.
Naibu
Waziri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mmanga Mjengo
Mjawiri pia ni Mwakilishi wa Jimbo las Mkanyageni akizungumza wakati wa
hafla hiyo na kumkaribisha Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema
Shein, kuzungumza na Wanafunzi wa Skuli hiyo.
Mke
wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia na kutowa
nasaha zake kwa Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua
alipofika kuwatembelea na kuwakabidhi vifaa kwa ajili ya matumizi yao ya
kila siku skulini hapo.
Wanafunzi
wa Kidatu cha Kwanza katika Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua
wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakati
alipofika kuwatembelea na kuwakabidhi misaada kwa ajili ya matumizi yao
skulini hapo.
Wanafunzi
wa Kidatu cha Kwanza katika Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua
wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakati
alipofika kuwatembelea na kuwakabidhi misaada kwa ajili ya matumizi yao
skulini hapo.
Mwalimu
wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua, Subira Othman Hafidh
akitowa neno la shukrani kwa Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema
Shein, na Ujumbe wake wa Wake wa Wawakilishi na Wabunge wa CCM kwa
msaada wao na umewafikia wakati muafaka.
Mwananchi
wa Kijiji cha Mkanyageni akisoma dua baada ya kumalizika kwa hafla hiyo
ya kukabidhi vifaa kwa Wanafunzi wa Skuli hiyo.
Mke
wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi mashine ya
kufulia nguo Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua
Mwalimu Ali Simai Makame, kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Mama Asha Suleiman.
Mke
wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi sabuni Mwalimu
Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua Mwalimu Ali Simai
Makame, kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha
Suleiman.na kulia Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe
Mmanga Mjengo Mjawiri.
Mke
wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi risiti ya vifaa
hivyo Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua Mwalimu
Ali Simai Makame, kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Mama Asha Suleiman.na kulia Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Mmanga Mjengo Mjawiri.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema
Shein akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya
Mohammed Juma Pindua Wilaya ya Mkoani Pemba. baada ya kumaliza hafla ya
kukabidhi vifaa kwa wanafunzi wa Skuli hiyo.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blog
Zanzinews.com.
0 Comments